Sunday, January 13, 2013

RUBANI WA UFARANSA AULIWA MAPIGANI YA MALI


Rubani wa Jeshi la Anga la Ufaransa ameuawa katika mapigano makali na waasi nchini Mali. Waziri wa Ulinzi Ufaransa Jean-Yves Le Drian ametoa ripoti ya kuuawa rubani huyo wa helikopta na kumtaja kuwa Luteni Damien Boiteux ambaye alipoteza maisha katika mapigano na waasi katika mji wa Konna. Huyo ndie afisa wa kwanza wa Jeshi la Ufaransa kuuawa tokea nchi hiyo ya Ulaya ijiingize rasmi kijeshi katika mgogoro wa Mali siku chache zilizopita. Ufaransa pia imepata pigo baada ya wanajeshi wake  wawili kuuawa katika mapigano ya hivi karibuni Somalia.
Waasi nchini Mali wanapinga uingiliaji wa nchi za kigeni katika mgogoro wa nchi hiyo na wamesema hawataweka chini silaha maadamu vikosi vya nchi za Ulaya na Marekani vinahusika katika mapigano nchini humo. Mgogoro uliibuka mali pale Rais Amadou Toumani Toure alipotimuliwa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi Machi 22 mwaka 2012. Baada ya mapinduzi hayo waasi walichukua udhibiti kamili wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO