Thursday, January 10, 2013

KAMANDA WA MAJESHI YA MAREKANI ULAYA AAPISHWA

Kamanda mpya wa wanajeshi wa Marekani barani Ulaya, Luteni Jenerali Donald M. Campbell, ameapishwa rasmi katika kambi mpya ya jeshi hilo, ya mji wa Ujerumani, Wiesbaden. Campbell tayari amedokeza kuhusu mipango ya kupunguza jeshi la Marekani linalohudumu barani Ulaya kutoka 40,000 hadi 30,000. Kwa sasa wanajeshi hao wanahama kutoka mji wa Haidelberg kwenda Wiesbaden, ambao uko karibu na uwanja wa kimataifa wa Frankfurt. Mpango huo wa uhamisho unatarajiwa kukamilika mnamo mwaka wa 2015.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO