Thursday, January 10, 2013

HAMAS NA FATAH WAAFIKIANA

Maafisa nchini Misri wamesema viongozi wa makundi ya Kipalestina, Hamas na Fatah, wamekubali kuanza kuutekeleza mpango wa amani ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu. Rais wa chama cha Fatah Mahmoud Abbas na kiongozi wa Hamas, Khaled Meshaal, wamekutana mjini Cairo jana, lakini hata hivyo, bado haijawa wazi kama makubaliano hayo yanakwenda mbali na kufanya mazungumzo zaidi. Hamas ililiteka  kwa nguvu eneo la Ukanda wa Gaza kutoka mikononi mwa Fatah mnamo mwaka wa 2007. Pande hizo mbili zilishindwa kuutekeleza muafaka uliotiwa saini mjini Cairo mwezi Mei mwaka wa 2011, ili kuunganisha uongozi wa ardhi ya wapalestina ambayo sehemu inakaliwa kimabavu na Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO