Rais wa Marekani Barack Obama amemteua Chuck Hagel jana kuiongoza wizara ya ulinzi, na hatua hiyo inaelekea kuzusha mvutano mkubwa katika hatua za kumuidhinisha wakati wapinzani kutoka chama cha Republican , wamesema amekuwa na msimamo mkali zaidi kwa Israel na amekuwa na mtazamo usio mkali dhidi ya Iran. Chaguo la Obama kwa John Brennan kuchukua nafasi ya David Patraeus kama mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA linaonekana kuwa halitakuwa na matatizo licha msimamo wa kiongozi huyo katika kuunga mkono mbinu za usaili na vita vinavyotumia ndege zisizo na rubani.Akimsifu Brennan rais Obama amesema.
O-Ton Obama
Mabadiliko ya kikosi cha rais Obama katika idara ya usalama wa taifa yanaonekana yataidhinishwa , lakini wabunge waandamizi wa chama cha Republican wameashiria kuwa haitakuwa rahisi kwa Hagel kupita licha ya kuwa anatoka katika chama hicho.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO