Lebanon itaendelea kuufungua mpaka wake na Syria kwa ajili ya kuwapokea wakimbizi, lakini itaomba msaada zaidi kutoka kwa mataifa ya Kiarabu na jamii ya kimataifa. Baraza la mawaziri limekataa miito ya mawaziri wa vuguvugu la Uzalendo Huru (Free Patriotic Movement), la kufunga mpaka wake huku idadi ya wakimbizi wa Syria walioko nchini Lebanon ikifika watu 125,000, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, na 200,000 kulingana na makadirio ya serikali.
Wakati huo huo, nchini Syria kwenyewe, watu wasiopungua tisa wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha petroli katika mji mkuu Damascus. Kwa mujibu wa taarifa, watu wengine 40 walijeruhiwa kutokana na shambulio hilo. Hii ni mara ya pili mnamo wiki hii kwa kituo cha petroli kushambuliwa. Wanaharakati wamedai kwamba watu kadhaa waliuawa baada ya ndege kushambulia, wakati walipokuwa katika foleni kwenye kituo cha petroli.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO