Saturday, January 05, 2013

MAREKANI KUIVAMIA IRAN NI KOSA KUBWA

Zbigniew Brzezinski Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesema kuwa, ni kitendo cha kijinga kwa Marekani kuendeleza chokochoko za vita dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa, kadhia ya nyuklia ya Iran inapasa kujadiliwa kwenye vikao vya Baraza la Seneti la nchi hiyo. Brzezinski ameitaka Kamati ya Uhusiano wa Kigeni ya Seneti ya Marekani kujadili kwa kina nafasi na ushawishi wa Iran katika matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla. Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani ameongeza kuwa, suala la vita au amani dhidi ya Iran liangaliwe kwa umakini mkubwa, sanjari na kuzingatiwa  maslahi ya Marekani. Amesema kuwa, ni suala lenye utata mkubwa la kuanzisha vita dhidi ya Iran kwani Washington haijui radiamali itakayotolewa na serikali ya Tehran baada ya nchi hiyo kushambuliwa. Mshauri huyo wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesisitiza kuwa, bila shaka shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran litasababisha hali kuwa mbaya zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla hivyo Washington haipaswi kufuata kibubusa ushauri wa kujitosa kwenye vita hivyo vya kihistoria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO