Saturday, January 05, 2013

MAREKANI YABANA VYOMBO VYA HABARI VYA IRAN


Marekani imeiwekea Iran vikwazo vipya ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku vyombo vyake vya habari katika hatua inayoenda kinyume na madai ya Washington ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari. Katika mswada mpya wa sheria ya vikwazo dhidi ya Iran uliotiwa saini Jumatano na Rais Barack Obama, Marekani imeliwekea rasmi vikwazo Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB na mkuu wake Sayyed Ezzatollah Zarghami. Aidha kwa mujibu wa mswada huo Marekani itasimamisha mali zote za IRIB na kuwazuia watu wengine kufanya biashara na shirika hilo la utangazaji la Iran. Vikwazo vya Marekani dhidi ya IRIB ni moja kati ya njama za nchi za Magharibi za kunyamazisha vyombo vya habari vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hivi karibuni mashirika ya Satalaiti ya Eutelsat SA, Intelsat SA, Hispasat na AsiaSat yalifuta kanali zote za televisheni na radio za Iran kufuatia mashinikizo ya nchi za Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.
Vyombo vya habari vya Iran vinasambaza habari za hakika na hivyo kuwavutia wengi duniani jambo ambalo limewakasirisha sana watawala wa nchi za Magharibi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO