Saturday, January 05, 2013

TALIBAN WAAHIDI MAPAMBANO BAADA YA 2014

Kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghnistan leo limeahidi umwagaji damu zaidi ikiwa vikosi vya Marekani vinavyolinda amani vitaendelea kubakia baada ya muda wa mwisho wa kuondoka majeshi ya kigeni mwaka 2014. Tangazo hilo la Taliban linatolewa wakati huu ambapo Rais Hamid Karzai wa Afghanistan akijiandaa kukutana na Rais Barack Obama wa Marekani mjini Washington wiki ijayo. Kundi la Taliban linasema kuwa kuwepo kwa vikosi vya Marekani nchini humo ndiyo chanzo cha vurugu na machafuko na hivyo Wamarekani ndio wanaopaswa kuathirika zaidi na hali hiyo. Afghanistan na Marekani zinajadiliana kuhusu mkataba wa ulinzi mara vikosi vya kigeni vitakapoondoka. Suala hilo ndilo mada kuu ya mazungumzo ya Obama na Karzai kuanzia Jumanne hadi Ijumaa wiki hiyo. Makubaliano hayo yataruhusu baadhi ya vikosi vya kijeshi vya Marekani kuendelea kushikilia kambi za jeshi nchini Afghanistan baada ya kuondoka kwa vikosi vya kigeni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO