Malala Yousafzai msichana mwenye umri wa miaka 14 raia wa Pakistan ameruhusiwa kutoka hospitali ya Queen Elizabeth ya mjini Birmingham nchini Uingereza baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani kwenye shambulio lililofanywa na kundi la Tehrik - Taleban mwezi Oktoba mwaka jana katika mji wa Mingora ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Malala alishambuliwa na kundi la Tehrik - Taleban kutokana na kosa eti la kuwashajiisha wasichana na wanawake wa Kipakistani kujiendeleza zaidi kimasomo. Mwanaharakati huyo wa Kipakistani alikimbizwa hospitalini nchini Uingereza ambako mara kadhaa alifanyiwa upasuaji kichwani mwake. Wakati akiwa amelazwa hospitalini nchini Uingereza, viongozi na shakhsia kadhaa wa Pakistan akiwemo Rais Asef Ali Zardari wa nchi hiyo walikwenda kumjulia hali yake. Mwaka 2008 na 2009 kundi la Tehrik Taleban liliwazuia wanawake wa Bonde la Swat katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa kujitafutia elimu na kusababisha wanawake 40,000 wa eneo hilo kukosa elimu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO