Pamoja na Ufaransa kuyashambulia maeneo ya Gao na Timbuktu nchini Mali bado waasi wanaendelea kuudhibiti mji wa Diabali wa nchi hiyo. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Drian amethibitisha kuwa, askari wa nchi yake, wameshatekeleza mashambulizi makali dhidi ya miji hiyo iliyotajwa. Aidha waziri huyo wa ulinzi amesema kuwa, pamoja na kuwepo katika mji wa Diabali askari wa wa Ufaransa na wa Mali, lakini bado mji huo unadhibitiwa na waasi. Siku 10 zilizopita Ufaransa ilianzisha mashambulizi yake dhidi ya waasi wanaoyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali, mashambulizi ambayo yametafsiriwa na weledi wengi wa masuala ya kisiasa kuwa, ni kinamasi kikubwa ilichojitumbukiza ndani Paris. Wakati huo huo duru za habari zinaarifu kuwa, Paris imeweka marufuku kali dhidi ya vyombo vya habari vinavyotangaza matukio yanayojiri katika vita hivyo dhidi ya waasi wa Mali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO