Sunday, January 13, 2013

WATU SABA WAUAWA NCHINI AFGHANISTAN


Polisi nchini Afhanistan imesema watu saba wameuwawa baada ya bomu moja kuripuka ndani ya msikiti wakati wa mapambano kati ya vikosi vya jumuiya ya NATO na waasi wa Taliban katika wilaya ya Sayed Abad kusini Magharibi mwa mji wa Kabul.
Kulingana na msemaji wa gavana wa eneo hilo Shahidullah Shahid majeshi ya serikali pamoja na yale ya NATO yalikuwa yanarudi kambini wakati waliposhambuliwa na waasi waliokuwa wamejificha ndani ya msikiti. Katika mashambulizi hayo waasi wanne waliuwawa na wakati wakaazi walipokuwa wakitoa miili ndani ya msikiti bomu likaripuka na kuwauwa watu saba. Hata hivyo polisi wanasema bado haijawa wazi iwapo mripuko huo umesababishwa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyejiripua ndani ya msikiti au kutokana na mabomu mengine.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO