Sunday, January 13, 2013

MAHAKAMA YA MISRI YATAKA KESI YA MUBAARAK ISIKILIZWE TENA


Mahakama Kuu nchini Misri imekubali ombi la aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak kukata rufaa dhidi ya kifungo cha maisha alichopewa baada ya kupatikana na makosa ya kusababisha mauaji ya waandamanaji katika maandamano ya kutaka mageuzi yaliomlazimisha kuachia madaraka. Rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo hicho mwezi Juni mwaka uliopita kwa kushindwa kuzuwiya mauaji ya raia 900 katika maandamano ya siku 11 yaliokomesha utawala wake wa miaka 29. Watu 6000 walijeruhiwa katika maandamano hayo. Mubarak aliondolewa madarakani mnamo mwezi wa Februari mwaka wa 2011.
Akitoa hukumu hiyo Jaji Ahmed Ali Abdel-Rahman pia alikubali kesi ya kukataa rufaa ya mkuu wa usalama katika serikali ya Mubarak Habib el-Adly ambaye hata yeye alihukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa kama ya Mubarak. Kama vile ilivyo kwa Mubarak yeye pia kesi yake itasikilizwa upya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO