Wednesday, January 16, 2013

WAZIRI MKUU WA PAKISTAN KUFUNGULIWA MASHITAKA

Serikali ya Pakistan imesema kuwa haijajulishwa kwa maandishi juu ya hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu Raja Pervez Ashraf, ambayo imetolewa na mahakama kuu ya nchi hiyo kuhusiana na tuhuma za rushwa dhidi ya Ashraf. Waziri mmoja wa Pakistan amesema watasubiri hati rasmi ya kukamatwa kwa waziri mkuu kabla ya kutoa tamko lolote, lakini alisema kuna uhusiano kati ya suala hilo na maandamano yanayoongozwa na kiongozi wa kiislamu mwenye ushawishi mkubwa, ambaye anataka bunge livunjwe. Kiongozi huyo, Tahir ul-Qadri amesema maandamano yao yananuia kuikomboa nchi. Waziri huyo amesema kulingana na maelezo aliyokuwa nayo, jina la waziri mkuu haliko kwenye orodha ya mahakama kuu, na kuongeza kuwa suala hilo limetiwa chumvi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO