Tuesday, July 16, 2013

NETANYAHU ATAKA KUANZA MAZUNGUMZO NA WAPALESTINA

Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameutumia kama kisingizio mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa shabaha ya kuwashinikiza na kuwalazimisha viongozi wa Palestina kushiriki kwenye meza ya mazungumzo ya amani. Taarifa zinasema kuwa, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amezungumza kwa njia ya simu na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na licha ya kumpongeza kwa kuanza kuingia mfungo wa mwezi wa Ramadhani, amemtaka arejee haraka iwezekanavyo kwenye meza ya mazungumzo kati ya Wapalestina na Wazayuni.
Hii ni mara ya kwanza kwa Netanyahu kuzungumza na Mahmoud Abbas, tokea  Netanyahu alipopewa jukumu la kuunda baraza jipya la mawaziri huko Israel. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mazungumzo ya amani kati ya pande mbili yalikwama baada ya utawala wa Israel kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye maeneo ya Wapalestina, na hata juhudi za Marekani za kuishinikiza Palestina irejee kwenye mazungumzo hayo zimegonga ukuta.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO