Wednesday, January 16, 2013

TIMU YA IAEA YAELEKEA IRAN


Timu ya umoja wa mataifa inaelekea Iran kuanzisha upya uchunguzi juu ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo. Kiongozi wa timu hiyo Herman Nackaerts amesema shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki IAEA linakamilisha mpango utakaobainisha yale linaloweza kuyafanya katika uchunguzi wake, na yale ambayo haliyawezi.
IAEA imejaribu kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzisha uchunguzi uliokwama, kuhusu shutuma kwamba Iran inajaribu kuunda bomu la nyuklia. Iran imekanusha vikali shutuma hizo, na imesisitiza kwamba shirika lolote linalozifanyia uchunguzi shutuma hizo, linapaswa kufanya hivyo chini ya makubaliano yanayoelezea mpaka wa uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO