Assalam Alaykum Warahmatul Lahi Wabarakatuh.
Jumuiya ya wanafunzi wa kiislam Muhimbili inachukua nafasi hii kwa kushikiana na Radio Imaan kuwatangazia waislam na wananchi wote juu ya msiba wa mlinganiaji na Sheikh wetu kipenzi mjuzi wa Ilmu Sheikh Nassor Bachu.
Taarifa ya msiba huo imethibitishwa na mtoto wake wa kiume Khamis Nassor Bachu ambaye amesema kuwa alikuwa amempakata mapajani mwake wakati sheikh anakata roho na kuwa marehemu Sheikh wetu kipenzi amefariki majira ya saa sita mchana Unguja nyumbani kwake. Taarifa juu ya mazishi ni kuwa kesho majira ya saa nne asubuhi huko donge msikiti wa KIKWAJUNI.
Masheikh mbalimbali wanawasili kutokea nchi mbalimbali na kuelekea huko zanzibar.
Mola ailaze mahala pema peponi Roho ya shekhe wetu kipenzi Sheikh Nassor Bachu.
"kila nafsi itaonja umauti na kwangu mutarejea"SURAT AL A'NKABUT 59.
Hakika sisi sote ni wenye kurejea n kwa mola na mola awape subira waumini wote hususani ndugu wa karibu na watoto wake wote. Hakika kama ingelikuwa ni kubaki baki angebaki kipenzi cha Allah mtume Muhammad Swallal lahu alayhi wasallam. Na iwapo yeye ametangulia basi hakuna mwenye kubaki katika dunia hii na pia kama ishara ya kukaribia Siku za mwisho wa dunia ni kufariki kwa masheikh wakubwa.
Mola alitanue kaburi lake na atujaalie tuweze kuienzi elimu aliyotuachia.
...........aamin aamin aamin...........
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO