Dakta
Muhammad Sarafraz Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa Shirika la
Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema kuwa, mfumo wa Kizayuni
unadhibiti kanali zote za habari ulimwenguni. Akizungumzia vita vipya dhidi ya
vyombo vya kupasha habari vya Iran, Dakta Sarafraz amesema kuwa, iwapo
itaanzishwa kanali ya habari itakayokuwa tofauti na kanali nyinginezo,
bila shaka mfumo wa Kizayuni utaingilia kati na kuifuta kanali hiyo.
Ameongeza kuwa, tarehe 28 Januari 2013 serikali ya Uhispania ilichukua maamuzi
yanayokinzana wazi na uhuru wa kujieleza pale ilipotoa amri ya kukatwa
matangazo ya kanali ya HispanTV ya Iran inayotangaza matangazo yake kwa lugha
ya Kihispania. Dakta Sarafraz ameongeza kuwa, sehemu ya hisa ya shirika la
huduma za satalaiti la Hispasat inafungamana na shirika la Eutelsat; na
Mkurugenzi wa Eutelsat ni Mfaransa mweye asili ya Kizayuni ambaye hivi karibuni
amekuwa akivisakama vyombo vya kupasha habari vya Iran huko Ulaya. Mkurugenzi
wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa IRIB ameongeza kuwa, Marekani inajidai
kuwa ni mtetezi mkubwa wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na demokrasia,
amma inawaunga mkono madikteta wa Bahrain na Saudia Arabia katika kuwakandamiza
wananchi wa nchi hizo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO