Wanamgambo wa muungano wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefyatuliana risasi na majeshi ya Cameroon katika mpaka wa nchi hizo mbili, na kusababisha wakazi wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao. Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yalianza siku ya Jumanne na bado yanaendelea katika eneo la Garoua- Boulaimashariki mwa Cameroon. Serikali ya Cameroon iliongeza idadi ya askari wake kwenye eneo la mpakani, mara baada ya kuanza machafuko katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mara kadhaa wamelalamikia mwendelezo wa vitendo vya wanamgambo wa Seleka wa kufanya mauaji, ubakaji na uporaji wa mali za wananchi mara baada ya kuiangusha serikali ya Francois Bozize wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO