Tuesday, March 05, 2013

ALQAEDA WATHIBITISHA KUUWAWA KWA KIONGOZI WAKE NCHINI MALI

Chanzo kutoka mtandao wa Al-qaeda kimethbitisha leo, kuwa moja wa viongozi wake wa tawi la Afrika Magharibi katika operesheni inayoongozwa na wanajeshi wa Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu nchini Mali. Mpiganaji wa kundi la AQIM ameliambia shirika la habari la Sahara Media la nchini Mauritania, kuwa kiongozi wa AQIM, Abdelhamid Abou Zeid, aliuawa katika shambulio la majeshi ya Ufaransa katika milima ya Ifoghas. Chanzo hicho lakini kilisisitiza kuwa kiongozi mwingine wa kundi la Kiislamu, Mokhtar Belmokhtar, bado ni mzima na anaendelea kupambana. Hii inapingana na madai kutoka Chad kuwa wanajeshi wake walimuua kiongozi huyo wa mashambulizi dhidi ya kiwanda cha gesi nchini Algeria mwezi Januari, yaliyouwa mateka 37 wa kigeni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO