Tuesday, March 05, 2013

VISA VYA WANAJESHI WA UINGEREZA NCHINI IRAQ KUCHUNGUZWA

Tume ya uchunguzi iliyosubiriwa kwa muda mrefu imezinduliwa nchini Uingereza, kuchunguza madai kuwa wanajeshi wa nchi hiyo waliwaua raia zaidi ya 20 nchini Iraq, miaka tisa iliyopita. Uchunguzi huo wa Al-Sweady, uliopewa jina la moja wa watu waliouawa, Hamid Al-Sweady mwenye umri wa miaka 19, utapitia madai kuwa wanajeshi wa Uingereza waliua wafungwa kufuatia makabiliano ya kurushiana risasi katika kizuizi mkoani Maysan, kusini mwa Iraq mwezi Mei mwaka 2004. Raia 15 wa Iraq watasafiri kwenda nchini Uingereza kutoa ushahidi mbele ya tume hiyo, akiwemo baba mdogo wa Al-Sweady, Khuder Al-Sweady na wafungwa wengine. Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema tayari imeshalipa fidia katika madai 227 ya ukiukaji wa haki za binaadamu uliyodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Uingereza kati ya mwaka 2003 na 2009, na kulipa jumla ya pauni milioni 15, ambazo ni sawa na dola milioni 23.7.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO