Friday, March 08, 2013

ALSHABAB WATAKAOJISALIMISHA KUJIUNGA NA JESHI LA SOMALI

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema yuko tayari kuwajumuisha wanachama wa kundi la Al-shabab katika jeshi la taifa iwapo wataamua kuweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali. Rais Hassan amesema nchi inamhitaji kila Msomali ili iweze kusimama wima na kujiunga tena na nchi zingine za dunia. Kiongozi huyo pia amelishukuru Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuiondolea nchi yake vikwazo vya silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema fursa hiyo itaiwezesha Mogadishu kujiimarisha zaidi kiusalama. Rais Hassan pia amezungumzia hali ya taasisi muhimu nchini Somalia na kusema kuwa baadhi ya taasisi kama vile idara ya mahakama ni dhaifu na ameitaka jamii ya kimataifa kusaidia kuinua hadhi ya taasisi hizo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO