Tuesday, March 05, 2013

ASKARI MWINGINE WA UFARANSA AUWAWA MALI

 Maofisa wakuu wa Jeshi la ufaransa wamesema mwanajeshi wao mmoja wa kikosi cha askari wa myamvuli ameuawa katika operesheni kubwa iliyofanyika katika boma walikokuwa wamejificha magaidi kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu karibu na mji wa Tessalite kaskazini mwa Mali. Mshauri wake mkuu wa majeshi ya Ufaransa anayehusika na mawasiliano Kanali Thierry Burkhard,amesema wanajeshi wa Ufaransa walikuwa wameteketeza sehemu kubwa ya ngome ya wapiganaji wa kigaidi katika eneo hilo.

Serikali ya Ufaransa imesema kuwa mwanajeshi huyo aliyeuawa ni Koplo Cédric Charenton,mwenye umri wa miaka 26,na kuwa huyu atakuwa ni mwajeshi wa tatu kuuawa katika kipindi cha miezi miwili na nusu tangu nchi hiyo kuingilia kijeshi mgogoro wa Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO