Watu wasiopungua 30 wamefariki dunia kwenye ajali ya ndege ya abiria iliyotokea huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa zinasema kuwa, ndege hiyo aina ya Fokker ilianguka wakati ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Goma mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa za awali zinasema kuwa, ndege hiyo iliyoanguka karibu na eneo la makazi ya watu, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo. Taarifa hizo zimeeleza kuwa, ndege hiyo ilikuwa ikitokea eneo la Kasai Mashariki lililoko katikati mwa Kongo na kuelekea katika mji wa Goma.
Ajali za kuanguka ndege nchini Kongo zimekuwa nyingi mno na mashirika yote ya ndege yapatayo 50 nchini humo, yamepigwa marufuku kufanya safari katika nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO