Polisi
ya Misri imesema kuwa imemtia mbaroni binamu na aliyekuwa mpambe wa karibu wa
Muammar Gaddafi kiongozi wa zamani wa Libya. Hapo jana maafisa wa Misri
walisema kuwa Ahmed Gaddaf al Dam alitiwa nguvuni baada ya vikosi vya usalama
kuizingira nyumba yake katika kitongoji cha Zamalek huko Cairo. Afisa mmoja wa
Misri amesema kuwa afisa huyo wa zamani wa intelijinsia wa utawala wa Gaddafi
atakabidhiwa kwa maafisa wa Libya hivi karibuni. Baada ya kuzingirwa nyumba
yake kwa masaa kadhaa huko katikati mwa Cairo, binamu huyo wa Muammar Gaddafi
alisikika akizungumza na kanali moja ya televisheni kwa njia ya simu na hapa
ninamnukuu" tulifika hapa kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri
na baraza la kijeshi, sisi si magaidi wa kuweza kushambuliwa namna hii,"
mwisho wa kumnukuu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO