Serikali ya Uingereza imetangaza rasmi kuwa itawapatia waasi wa Syria zana za kijeshi ili kupambana na majeshi ya serikali ya nchi hiyo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uingereza William Hague ameliambia rasmi bunge la nchi hiyo kuwa, London itawatumia silaha waasi wanaopigana na serikali ya Rais Bashar Assad wa Syria. Hague ameongeza kuwa, zana na silaha hizo za kijeshi zitakazotumwa kwa waasi nchini Syria zina thamani ya paundi milioni ishirini. Hague amesema kuwa, misaada ya kijeshi kwa wapinzani na waasi wa serikali ya Syria ni jambo lenye umuhimu mkubwa.
Hivi karibuni pia Marekani ilitangaza kuwa iko tayari kuwapatia dola milioni sitini waasi wanaopigana na serikali ya Syria. Nchi za Magharibi na hasa Marekani, Uingereza na Ufaransa na zile za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na Uturuki zinatumia waasi wa Syria misaada ya kijeshi na kifedha kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo. Serikali ya Rais Bashar Assad inasakamwa na nchi za Magharibi na Kiarabu kutokana na misimamo yake imara dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuyaunga mkono makundi ya mapambano ya Kipalestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO