Tuesday, March 05, 2013

SOMALIA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ALSHABAB


Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia ametangaza kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na kundi la wanamgambo wa al Shabab la nchini humo. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Doha Qatar, Rais Hassan Sheikh amesema kuwa, mazungumzo hayo hayatawashirikisha wanamgambo ambao  wanasakwa na taasisi za kimataifa au wanaokabiliwa na tuhuma za kutenda jinai za kivita. Aidha Rais wa Somalia amesema kuwa, amefanya mazungumzo na Amir wa Qatar juu ya masuala yanayohusu mahusiano ya pande mbili, kieneo na kimataifa.
Kundi la wanamgambo wa al Shabab linalofungamana na mtandao wa al Qaeda linadhibiti baadhi ya maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia, na mara kadhaa limekuwa likipambana na vikosi vya serikali na vile vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO