Saturday, March 09, 2013

NICOLAS MADURO AAPISHWA KUWA RAIS WA VENEZUELA

Nicolas Maduro ameapishwa kuwa rais wa muda wa Venezuela, saa chache baada ya kuhitimishwa kwa msiba wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Hugo Chavez, katika ibada iliyofanyika katika Chuo cha Kijeshi mjini Caracas. Hata hivyo, upande wa upinzani umesema kuapishwa kwa Maduro kumekiuka katiba, ambayo inasema ni spika wa bunge aliestahili kukaimu urais. Maduro ameitaka tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi mpya haraka, na kuwatahadharisha wapinzani dhidi ya kuususia.Viongozi kadhaa wa dunia walihudhuria msiba wa Chavez, wakiwemo marais wa Iran, Mahmoud Ahmadnejad, na Raul Castro wa Cuba. Maelfu ya waombolezaji pia walijipanga katika mitaa nje ya chuo cha kijeshi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wao wa miaka 14. Chavez alifariki siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 58, baada ya kuungua ugonjwa wa saratani kwa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO