Saturday, March 09, 2013

VIKOSI VYA USALAMA BAHRAIN VYAWATESA WANAWAKE

Kanali ya Televisheni ya al Manar ya nchini Lebanon imeripoti kuwa,  wanawake 11 wameuawa shahidi  katika  harakati za mapinduzi ya wananchi wa Bahrain, na wengine 230 wanakabiliwa na mateso na ukandamizaji mkubwa  kwenye jela za kuogofya za utawala wa Aal Khalifa nchini humo. Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya tarehe 8 Machi ya kila mwaka kuwa ni siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Bahrain wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha na kukiukwa  haki zao nchini humo. Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Bahrain imeeleza kuwa, mara baada ya kuanza harakati za kimapinduzi nchini humo mwezi Februari mwaka 2011, mashinikizo makubwa yaliwekwa dhidi ya wanawake na haki zao zimekuwa zikikanyagwa siku hadi siku. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumla ya wanawake 230 hivi sasa wanashikiliwa ndani ya jela za Bahrain wakikabiliwa na mateso makubwa ya kupigwa na hata kuchomwa  vitu vyenye ncha kali. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanawake na watoto wadogo walipoteza maisha kwenye maandamano baada ya kurushiwa mabomu yenye gesi ya sumu na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO