China imetaka kuewepo na utulivu baada ya Korea Kaskazni kutangaza kufuta makubaliano yote ya amani na Korea Kaskazini. China kama mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, imezikata pande zote mbili kufanya mazungumzo na kuonda mvutano uliyopo. Hatua hiyo ya Korea Kaskazini inatokana na uamuzi wa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo vikali Korea Kaskazini vikilenga uchumi wa nchi hiyo na viongozi wake.Hatua hizo za vikwazo zimeandaliwa na Marekani na China baada ya nchi hiyo kufanya jaribio lake la tatu la nuklea mwezi uliopita.
Kabla ya kuidhinishwa kwa vikwazo hivyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Alhamisi Korea Kaskazini pia iliitishia kuishambulia Marekani kwa kombora la nuklea.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO