Friday, March 22, 2013

UCHUNGUZI WA SILAHA ZA KIKEMIA WAANZA SYRIA

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema Umoja huo utachunguza ikiwa kuna matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria. Ban amesema matumizi ya silaha kama hizo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na kwamba anafahamu kuwa kuna madai ya kutokea mashambulio kama hayo. Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Matifa amesema anatumai kuwa uchunguzi huo utasaidia kuhifadhi silaha hizo za kemikali nchini Syria. Wachunguzi watachunguza madai ya serikali ya Syria kuwa waasi walitumia silaha za kemikali hatari kushambulia kijiji cha Khan al Assal kaskazini mwa jimbo la Aleppo,madai ambayo waasi pia wananyoosha kidole cha lawama dhidi ya serikali. Wakati huo huo afisa mmoja wa ngazi za juu wa Marekani hapo jana alisema Marekani inaamini kuwa hakuna silaha za kemikali zilizotumika katika shambulio hilo la Aleppo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO