Serikali ya Rais Obama imeliwekea vikwazo kundi la kiislamu lenye itikadi kali la Ansar Diin ambalo lilidhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Mali mwaka jana. Wizara ya ulinzi ncini Marekani imeliorodhesha kama kundi la kigaidi na kuzuia mali zote ilizo nazo nchini Marekani na kuwapiga marufuku raia wa Marekani kujihusisha na biashara yoyote na kundi hilo. Marekani ilimuwekea vikwazo sawia na hivyo kiongozi wa kundi hilo Iyad Ag Ghali mwezi uliopita. Kwa usaidizi wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, Ansar Dine liliweza kuyadhibiti maeneo mengi ya kaskazini mwa Mali baada ya uasi wa makundi ya kikabila. Umoja wa Mataifa pia umeliwekea kundi hilo vikwazo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO