Watu wasiopungua 185 wameuliwa kaskazini mashariki mwa Nigeria katika
mapigano kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wapiganaji wa Boko Haram. Lewa
Kole afisa wa serikali za mitaa amemueleza gavana wa jimbo la Borno Kashin
Shettima kuwa mapigano yalianza Ijumaa iliyopita huko Baga katika jimbo la Borno
na kudumu kwa masaa kadhaa.
Hata hivyo bado haijafahamika ni askari, raia au wanamgambo wangapi wa Boko
Haram waliouliwa katika mapigano hayo kwa kuzingatia kuchomwa moto viwiliwili
vingi ambavyo havijaweza kutambuliwa, kufuatia moto ulioteketeza karibu mji huo
wote. Brigedia Jenerali Austin Edokpaye amesema kuwa raia wengi walitumiwa na
wapiganaji wa Boko Haram kama ngao ya binadamu katika mapigano hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO