Mwendesha mashtaka Mkuu nchini Misri, anakusudia kumpandisha kizimbani mtoto wa
ndugu wa dikteta aliyeuawa nchini Libya Kanali Muammar Gaddafi. Ahmed
GaddafAl-Dam atapandishwa katika mahakama kuu nchini Misri, kwa tuhuma za
kuanzisha mauaji, kupambana na askari wa usalama na kumiliki silaha kinyume cha
sheria. Itakumbuwa kuwa, tarehe 19 mwezi Machi mwaka huu, Ahmed GaddafAl-Dam
aliwafyatulia risasi Polisi wa Kimataifa Interpol na wa Misri na kumjeruhi mmoja
wao, katika oparesheni ya kumtia mbaroni mwana huyo wa ndugu wa Kanali Muammar
Gaddafi. Mbali na idara ya mahakama nchini Misri kupinga kumkabidhi Ahmed
GaddafAl-Dam kwa serikali ya Libya, imetangaza kumshitaki katika mahakama zake
huku ikiwa tayari imekwishatekeleza usaili dhidi yake
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO