Maandamano yanaendelea katika miji mbalimbali nchini Marekani kushinikiza Bunge la Congress kupitisha mswaada wa Uhamiaji, ambao utatoa nafasi kwa zaidi ya wahamiaji milioni 11 wasio na vibali nchini humo kupata uraia.
Maandamano hayo yalinuiwa kushinikiza bunge la Congress kuchukua hatua wakati maseneta wakijadiliana kuhusu mageuzi ya sheria za uhamiaji. Mswaada huo unaoandaliwa na Maseneta wa Marekani, unanuia kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mpaka wa Marekani na Mexico. Maelfu ya watu wamekusanyika mbele ya jengo la Capitol, mjini Washington, na wakereketwa wanasema kuwa maandamano sawa na hayo yameandaliwa katika majimbo mengine 18 nchini humo. Wengine zaidi ya elfu moja waliandamana mjini Atlanta.
Wabunge wanatarajiwa kuzindua mswaada ambao utawahalalisha wahamiaji wasio na stakabadhi kuwa raia halali wa Marekani. Shinikizo za mageuzi ya sheria ya uhamiaji yanakuja baada ya uchaguzi wa urais ambaye raia wahispania walimpigia kura kwa wingi rais Obama na wagombea wa democrats. Idadi kubwa ya wahamiaji takriban milioni moja nchini Marekani ni wenye asili ya Hispania, na wanachama wa Republican wanasema wameona bora kuunga mkono mageuzi ya uhamiaji ikiwa wanataka kushinda uchaguzi wowote.
Miongoni mwa waliaondamana siku ya Jumatano ni pamoja na wakulima, wafanyakazi wa nyumbani , viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanaharakati wa kutetea haki za wahamiaji.
''Hatuwezi kushinda katika shinikizo zetu za kutaka mageuzi ya sheria za uhamiaji kwa kuja hapa Washington,''alisema Ben Monterroso, mmoja wa wanaharakti. ''Tunahitaji kwenda sehemu nyingi za nchi.''
Waandalizi wa maandamano hayo, mjini DC walisema kuwa takriban mabasi 400 yaliwaleta watu mjini Washington, kutetea mageuzi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO