Tuesday, March 19, 2013

KOFFI ANNAN APINGA KUPEWA SILAHA WAPINZANI WA RAIS ASSAD

Koffi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kupatiwa silaha waasi wa Syria ndilo chimbuko kuu la kuvurugika zaidi hali ya mambo katika nchi hiyo ya Kiarabu na kushadidisha mgogoro huo. Annan ambaye aliwahi pia kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria, amepinga hatua yoyote ile ya kupatiwa silaha makundi ya waasi nchini Syria na kusisitiza kwamba, hatua hiyo haina natija nyingine ghairi ya kushadidisha mgogoro wa nchi hiyo na kuzorotesha zaidi hali ya amani na usalama. Kofi Annan ameashiria uamuzi wa baadhi ya nchi za Ulaya za kuwapatia misaada ya silaha waasi wa Syria na kusisitiza kwamba, kupatiwa silaha waasi hao katu hakuwezi kuboresha mambo. Ikumbwe kuwa, licha ya pingamizi na ukosoaji wa kieneo na kimataifa, hivi karibuni Ufaransa na Uingereza zilitangaza wazi kwamba, zitawaunga mkono waasi wa Syria na hata kuwaptia silaha waasi hao ambao wamekuwa wakiwauwa ovyo raia wasio na hatia wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO