Benki ya Dunia imesema kwenye ripoti yake mpya kuwa, uharamia wa baharini
nchini Somalia umesababisha kuongezeka gharama ya kuendesha biashara ya
kimataifa kwa zaidi ya dola bilioni 18 kila mwaka. Ripoti hiyo aidha imesisitiza
kuwa mfumuko wa bei za bidhaa muhimu pia umesababishwa kwa kiwango fulani na
tatizo la uharamia wa baharini katika pwani ya Somalia. Hata hivyo, Benki ya
Dunia imekiri kwamba uharamia umepungua mno katika kipindi cha miaka 2
iliyopita. Imesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za nchi mbalimbali
kupeleka wanajeshi wa majini kupiga doria katika maji ya kimataifa karibu na
pwani za Somalia na Aden. Mwaka 2009 zaidi ya meli 100 zilitekwa nyara na
maharamia huko Somalia jambo lililotoa pigo kubwa kwa biashara ya mafuta na
matunda katika soko la kimataifa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO