Watu waliokuwa na bunduki wamempiga risasi na kumuuwa mgombea mmoja katika uchaguzi nchini Pakistan, wakati vyama vya kisiasa vinavyokabiliwa na vitisho vya uasi vikijizatiti kuendelea na kampeni zao kabla ya uchaguzi wa Mei 11. Fakhr-ul-Islam, ambaye chama chake cha Vuguvugu la Mutahhida Qaumi, MQM, kinakabiliwa na vitisho kutoka kundi la Taliban nchini Pakistan kuhusiana na shutuma zake za uasi, ameuawa nje ya nyumba yake viungani mwa mji wa Hyderabad, Kusini mashariki ya Karachi. Kundi la Taliban limekiri kufanya mauwaji hayo. Marehemu alikuwa ametuma ombi la kugombea kiti katika bunge la Sindh. Maafisa wa uchaguzi wanatarajiwa kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea tarehe 19 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO