Mamia ya maelfu ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefanya
maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui wakiulalamikia muungano wa
waasi wa Seleka uliofanya mapinduzi nchini humo. Waandamanaji hao wamelalamikia
mauaji ya kiholela yanayofanywa na waasi hao wa zamani pamoja na uporaji wa
mali unaofanyika kwenye mji mkuu nchi hiyo. Arsene Ndirifei Mratibu wa taasisi
na asasi zilizoitisha maandamano hayo amesema kuwa, walikuwa wanataka kupeleka
miili ya wahanga kwenye hoteli anayoishi Michel Djotodia kiongozi wa wafanya
mapinduzi ili ajionee jinai zinazotendwa na wanamgambo wa muungano wa Seleka.
Mara baada ya kuangushwa serikali ya Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika
ya Kati, wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS
waliketi kwenye kikao cha dharura nchini Chad kuanzia tarehe Mosi hadi Pili
mwezi huu, na kuwataka waasi wa Seleka kuunda serikali ya mpito nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO