Wednesday, April 10, 2013

VISA VINAVYOWAKUTA WATOTO NCHINI SYRIA

Shirika la kutetea haki za watoto Save the Children, limekusanya maelezo ya kutisha na kuogofya kuhusu visa vinavyowakumba watoto katika vita vinavyoendelea nchini Syria. Shirika hilo limekusanya ushahidi kutoka kwa watoto waliotoroka vita na ambao wameelezea dhulma na mateso waliyokumbana nayo.  Kwa mujibu wa shirika hilo, kila mtoto aliyehojiwa na ambaye ameweza kutoroka Syria, ameelezea kuona jamaa wake angalau mmoja akiuawa.
Shirika hilo linasema kuwa limehoji mtoto mwenye umri wa miaka 15, aliyechomwa kwa sigara,wakati alipokuwa amefungwa katika iliyokuwa shule yake. Mtoto mwingine alizungumzia kupigwa na umeme huku akiishi katika chumba kimoja na maiti. Ingawa shirika hilo halikutoa taarifa rasmi kuhusu nani aliyetenda mateso hayo, limeisisitizia Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya wanaotenda dhulma hizo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO