Juhudi za kukomesha hukumu ya kunyongwa duniani zinaendelea
katika baadhi ya nchi licha ya nchi kadhaa kuanza tena kutekeleza hukumu hiyo
mwaka 2012. Hii ni kulingana na shirika la Amnesty International. Utekelezaji wa hukumu hiyo ulitokea nchini India, Japan, Pakistan na Gambia,
na hili lilikuwa jambo la kusikitisha kulingana na Amnesty. Lakini kwingineko, hukumu hiyo inaendelea kuwa jambo linalosahaulika. Alisema
katibu mkuu wa shirika hilo Salil Shetty . Nchi tano ambazo zimeripotiwa kutekeleza hukumu hiyo pakubwa, ni pamoja na
China, Iran, Iraq, Saudi Arabia, na Marekani
Amnesty International imeelezea kuwa na wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya
watu kunyongwa nchini Iraq - huku idadi ikiwa kubwa zaidi mwaka jana
ikilinagnishwa na mwaka 2011 kutoka 68 hadi 129. Shirika hilo liligindua kuwa nchini Iran mnamo mwaka 2012 takriban watu 314,
walinyongwa nchini na wengine 79 nchini Saudi Arabia. Marekani iliwanyonga watu 43 idadi sawa na walionyongwa mwaka 2011, ingawa
katika majimbo machache. Hata hivyo, hakuna idadi kamili ya walionyongwa inajulikana nchini China
ambako kuna usiri mkubwa.. Hata hivyo shirika hilo linaamini kuwa maelfu ya watu
walinyongwa, ikiwa idadi kubwa zaidi kuliko katika nchi yoyote duniani.
Aidha shirika hilo liligundua kuwa visa vya kutekeleza hukumu ya kunyongwa
vinashuka chini kote duniani licha ya idadi ya nchi zinazoanza kutekeleza hukumu
hiyo. India imetekeleza hukumu yake ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya mshukiwa
pekee aliyesalia wa mashambulizi ya mwaka 2008 mjini Mumbai. Nchini Indonesia ambako, mwanamke muingereza Lindsay Sandiford, anakabiliwa
na hukumu ya kunyongwa kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya, pia imetekeleza hukumu
yake ya kwanza ya kunyongwa katika kipindi cha zaidi ya miaka minne. Hata hivyo hili halikujumuishwa katika ripoti ya shirika la Amnesty.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO