Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wimbi la hamasa ya kisiasa, ni kuhudhuria wananchi wa Iran katika uchaguzi wa rais utakaofanyika hapa nchini. Rais Ahmadinejad ameyasema hayo leo mbele ya maelfu ya watu wa mji wa Semnan huko mashariki mwa Iran. Akiashiria sababu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuuita mwaka huu ulioanza wa Hijria Shamsia kuwa mwaka wa hamasa ya kisiasa na hamasa ya kiuchumi amesema hiyo ni kwa kuwa wananchi watakuwa na mchango mkubwa katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu. Uchaguzi wa 11 wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unatazamiwa kufanyika tarehe 13 Juni mwaka huu. Aidha akiashiria sababu ya kuitwa mwaka huu kuwa mwaka wa hamasa ya kiuchumi, Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa, uchumi wa taifa hili lazima ustawi zaidi na kuyashinda mashinikizo na vikwazo vya maadui wake. Ameashiria propaganda zisizo na ukweli wowote za maadui kwamba eti mashinikizo yameathiri uchumi wa taifa hili na kuongeza kuwa, Iran ya Kiislamu inaweza kuvuka vizingiti vyote vya maendeleo hasa kwa kuzingaztia kwamba, nchi hii inamiliki vyanzo vingi vya utajiri.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO