Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, Boko Haram ,
limekataa pendekezo la kukubali msamaha. Wiki jana Rais Goodluck Jonathan, aliuomba mkutano wa maafisa wakuu wa
usalama kutafakari swala la kuwapa msamaha wapiganaji hao ili kuwashawishi
kusitisha harakati zao. Tangazo na mtu anayeaminika kuwa kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau. Katika miaka ya hivi karibuni, Boko Haram imekuwa ikiendesha kampeini ya
ghasia na vurugu katika eneo la Kaskazini mwa nchi, na kuwaua takriban watu
2,000. Kundi hilo linasema kuwa wapiganaji wake wanapigania kile wanachosema ni
taifa la kiisilamu katika eneo la Kaskazini ambalo lina idadi kubwa ya
waisilamu.
Bwana Shekau alisema kuwa kundi lake halijakosa hata kidogo, na kwa hivyo
msamaha kwao sio jambo la kuzungumzia. Aidha Shekau aliongeza kuwa ni jeshi la Nigeria ambalo linakiuka haki za
waisilamu. "nashangazwa kwa kuwa serikali ya Nigeria inazungumzia kuhusu msahama. Sisi
tumefanya makosa gani? Ni sisi ambao tunapaswa kuwasamehe.'' alinukuliwa akisema
Shekau
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria,Will Ross, anasema kuwa viongozi wa kisiasa
na kidini Kaskazini mwa nchi, wamekuwa wakimtaka rais Jonathan kuwasamehe
wapiganaji hao, wakisema kuwa hatua za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao
hazisaidii kuleta amani. Jopo la kutoa msahama liliundwa na serikali wiki jana na linajumuisha
waakilishi wa jeshi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO