Kwa akali watu 13 wameuawa nchini Somalia na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab dhidi ya vikosi vya serikali na vile vya Ethiopia. Duru za usalama zinaripoti kutoka Somalia kwamba, mashambulio hayo yametokea katika eneo moja kusini magharibi mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Taarifa zaidi zinasema kuwa, wanamgambo wa al-Shabab wamefanya mashambulio makubwa dhidi ya vituo viwili vya vikosi vya serikali ya Somali na vile vya Ethiopia vinavyoisaidia serikali ya Mogadishu katika mji wa Bakool kusini magharibi mwa Somalia. Wote waliouawa katika mashambulio hao ni askari wa serikali ya Mogadishu. Msemaji wa al-Shabab Abdu Aziz Abu Muscab ameziambia duru za habari kwamba, miongoni mwa waliouawa katika mapigano hayo wamo wanajeshi watano wa serikali ya Somali na sita wa vikosi vya Ethiopia. Wakati huo huo, habari kutoka Somalia zinasema kuwa, hali ya usalama bado imeendelea kuzorota katika miji mbalimbali ya nchi hiyo licha ya juhudi za kieneo na kimataifa za kujaribu kurejesha amani na uthabiti katika nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO