Gazeti la Times linalochapishwa nchini Uingereza limeitaja dini tukufu ya Kiislamu kuwa ni dini yenye kutilia umuhimu mkubwa suala la kuwalingania watu katika kutoa walichonacho na kwamba wafuasi wa dini hiyo tukufu ndio watu wakarimu zaidi kati ya wananchi wa Uingereza. Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la Times kwa kushirikiana na kituo cha mawasiliano cha 'Just Giving' kwa watu elfu nne nchini Uingereza unaonyesha kuwa, Waislamu nchini humo ni wakarimu zaidi kuliko wafuasi wa dini nyingine. Imeelezwa kuwa, Waislamu wamekuwa wakitoa misaada yao ya kibinadamu kupitia taasisi kama vile 'Islamic Relief' na 'Muslim Aid' kwa watu wenye kuhitaji misaada na pia hupeleka misaada kwa taasisi zisizokuwa za Kiislamu kama vile taasisi za kusaidia wagonjwa wa maradhi ya saratani nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO