Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya dharura katika majimbo matatu ya kaskazini mwa nchi hiyo jana Jumanne. Tangazo hilo limetolewa katika juhudi za kukabiliana na vurugu zinazofanywa na kundi la Kiislamu la Boko Haram dhidi ya vikosi vya serikali. Katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia vituo vya redio na televisheni, Jonathan alisema wanajeshi watapelekwa mara moja katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa.
Chini ya sheria za Nigeria, rais ana mamlaka ya kuwaondoa wanasiasa katika nafasi zao na kuteuwa serikali ya mpito baada ya kutangaza hali ya dharura. Katika hotuba yake, Jonathan alisema wanasiasa wataendelea na nafasi zao. Tangu mwaka 2010, maelf ya watu wameuawa katika mashambulizi ya waasi hao wa Kiislamu, ambao wanataka utawala wa sheria nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO