Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema serikali yake inafanya kila iwezalo kuzuia silaha zinazotumiwa katika mgogoro wa Syria kuwafikia kundi la Hezebollah nchini Lebanon. Matamshi ya Netanyahu yamekuja wiki mbili baada ya Israel kufanya mashambulizi ya kutokea angani karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus, ambayo afisa mmoja wa ngazi ya juu wa jeshi la Israel alisema yalilenga kuzuia usambazaji wa silaha zilizotengenezwa Iran kulifikia kundi la Kishia la Hezbollah, ambalo ni mshirika wa Rais Bashar al Assad wa Syria. Netanyahu amesema kuwa eneo la Mashariki ya Kati linapitia kipindi kigumu kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa, huku mzozo wa Syria ukiwa kitovu cha machafuko hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO