Majeshi ya Syria yakisaidiwa na wapigananji wa kundi la Lebanon la Hezbollah leo yameshambulia na kuingia katika mji muhimu wa waasi wa Qusayr, siku moja baada ya Rais Bashar al-Assad kusisitiza kuwa hataachia madaraka. Hayo yanakuja wakati wapinzani wakionya kuwa shambulizi la kinyama na uharifu la utawala wa Assad, katika mji wa Qusayr huenda ukazifanya juhudi za pamoja za Marekani na Urusi kuandaa mkutano wa amani wenye lengo la kumaliza mzozo wa miaka miwili ya umwagaji damu nchini Syria, kuwa hazina maana. Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeitisha mkutano wa dharura siku ya Alhamisi, kabla ya mkutano huo, kufuatia madai ya kundi la upinzani la Baraza la Kitaifa la Syria - SNC, ya kuitaka jumuiya hiyo kukutana na kusitisha mauwaji ya kinyama mjini Qusayr. Takribani watu 30, ikiwa ni pamoja na wapiganaji waasi 16, wameuawa katika mapigano hayo, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binaadamu la Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO