Friday, May 10, 2013

ISRAEL YAHAHA BAADA YA SYRIA KUPANGA KUNUNUA KOMBORA LA S300 TOKA RUSSIA

Utawala haramu wa Kizayuni, Israel, umepatwa na wasiwasi mkubwa kutokana na hatua ya Russia kutaka kuiuzia Syria kombora la S 300. Israel imeitaka serikali ya Moscow kutoiuzia Damascus kombora hilo. Kombora la S 300 linatajwa kuwa na uwezo mkubwa na hivyo kuweza kuinua uwezo wa jeshi la Syria katika kukabiliana na uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya taifa hilo. Kabla ya hapo gazeti la The Wall Street Journal lilikuwa limeandika kuwa, Israel iliitahadharisha Marekani kwa kile ilichokisema kuwa, ni Syria kumiliki kombora la S 300 kutoka Russia. Aidha gazeti hilo liliongeza kuwa, makabidhiano ya kombora hilo yatakamilika ndani ya miezi mitatu ijayo. Kombora la S 300 lina uwezo wa kuangamiza ndege na kadhalika makombora ya umbali wa kilometa 200 na hivyo kuweza kuinua kabisa uwezo wa jeshi la ulinzi nchini humo. Wasiwasi wa Israel, unakuja katika hali ambayo siku ya Jumapili, ndege za utawala huo zilivuka anga ya Syria na kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo, suala lililoiba radiaamali za walimwengu za kulaani shambulio hilo.

1 comment:

  1. duh sio mchezo, naona tunaeleka kwenye vita vya tatu vya dunia sasa, Mungu atuepushe na hayo inshallah.

    ReplyDelete

TUPE MAWAZO YAKO