Nicolas Maduro Rais mteule wa Venezuela ameilaumu Marekani kwa kuchochea machafuko nchini humo. Maduro amesema kuwa ubalozi wa Marekani huko Caracas ulihusika kutokana na ghasia zote zilizotokea baada ya uchaguzi wa rais wa Jumapili iliyopita. Maduro amesema ubalozi wa Marekani mjini Caracas umekuwa ukifadhili kifedha na kuongoza machafuko yote na kuongeza kuwa ubalozi huo unaunga mkono kile alichokiita "Makundi ya Wanazi Mamboleo huko Venezuela."
Rais mteule wa Venezuela ameutuhumu pia mrengo wa upinzani nchini humo kwa kujaribu kufanya mapinduzi baada ya maandamano dhidi ya serikali katika siku mbili zilizopita na kupelekea watu saba kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO