Habari kutoka Syria zinasema kuwa jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuchukua udhibiti wa miji mitatu iliyokuwa mikononi mwa waasi katika mikoa ya Homs na Dara'a.
Habari zaidi zinasema jeshi hilo limewaua majangili kadhaa kwenye oparesheni hiyo. Wakati huohuo, serikali ya Syria imekanusha kuhusika na shambulio la bomu huko Uturuki ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa. Waziri wa Habari wa Syria, Omran al-Zohbi amesema serikali haiwezi kutenda ugaidi kama huo kwani imani na itikadi ya Kiislamu hairuhusu ugaidi. Baadhi ya vyombo vya habari vya Magaribi vimekuwa vikiripoti kwamba serikali ya Syria ndiyo iliyohusika na milipuko katika mji wa Reyhanii. Omran al-Zohbi amesema serikali ya Uturuki huenda ndiyo iliyopanga milipuko hiyo ili kuhalalisha uingiliaji wa kijeshi wa NATO nchini Syria. Kiongozi huyo amehoji ni kwanini milipuko hiyo imetokea siku chache kabla ya mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Uturuki na Rais wa Marekani?
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO